- Babu alichapisha picha yake ya awali akiwa kanisani ambapo amempigia magoti Mungu kunyenyekea
- Amekuwa akiomba msamaha na kusema yuko tayari kuanza mkondo mpya wa maisha
- Babu anakabiliwa na shtaka la kumpiga risasi mcheza santuri DJ Evolve walipokuwa kwenye klabu kimoja Kileleshwa
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino Jumapili, Agosti 2 alinyenyekea kwa Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha.
Babu alikiri mbele zake Bwana kuwa ni mwenye dhambi na kwa sasa anaomba kuchukua mkondo mpya kimaisha.
Habari Nyingine: Watu 10 waangamia baada ya kunywa kitakasa mikono kufuatia uuzaji wa pombe kupigwa marufuku
![](https://cdn.statically.io/img/cdn.tuko.co.ke/images/1120/37dc6b342ef2e4a4_w.jpeg)
Mbunge huyo alichapisha picha yake ya awali akiwa kanisani ambapo amepiga makogi kama njia ya kunyenyekea mbele zake Bwana.
"Mungu mimi ni mwenye dhambi, nakuomba unisamehe dhambi zangu," aliandika kwenye picha hiyo aliyochapisha kwenye Facebook.
Hatua ya Babu ilijiri siku chache tu baada ya kutangaza kuwa amegundua amekuwa akiishi maisha mabaya na yuko radhi kubadilika.
Habari Nyingine: Zawadi ya vijana wa Nyanza kwa Oscar Sudi yasisimua mtandao
Kwenye video aliyochapisha hapo awali, Babu alisema amegundua hulka zake zimekuwa zikiwakera Wakenya na akawataka kumsamehe.
Alisema ameamua kuwa kiumbe kipya na hata kuacha kushiriki mvinyo kama njia moja ya kuanza maisha mapya.
Alimshukuru mkewe akisema ameungana naye kwenye maombi na ili kuchukua mkondo mpya.
Habari Nyingine: Uasin Gishu: Binti awajengea wazazi wake nyumba ya kifahari kwa kumpa masomo mazuri
![](https://cdn.statically.io/img/cdn.tuko.co.ke/images/720/9eb798a7c95717f0.jpeg)
Mbunge huyo alisema hulka zake za ghasia zilitokana na jinsi alilelewa ambapo mamake alikuwa ni mgema kutokana na umaskini.
"Picha za mamangu na ndugu zangu wakikamatwa na polisi na hata kupewa kichapo zilinifanya nilivyo. Lakini niko tayari kuchukua mwelekeo mpya," alisema.
Babu amekuwa akikemewa sana na wengi haswa baada ya kisa ambapo alimpiga risasi DJ Evolve walipokuwa kwenye eneo la Burudani mtaani Kileleshwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbH53gpBmpKKlmWK7qnnMsJynsZVisamtzJugZqaZqK6usceeZJuvkaOubnmMm5ibrV2kxKq6zmaYp7GVo8amt8SaZKSvkWK6trrGrmWhrJ2h