- Aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi uliopita wa 2017 amemtaka Uhuru Kenyatta kulitaja baraza lake la mawaziri
- Aukot alisema kuwa Uhuru anafaa kuchukua mfano wa rais mwenzake wa Liberia, George Weah aliyelitaja baraza lake siku chache tu baada ya kuapishwa
Uhuru amezidi kukabiliwa na shinikizo za kulitaja baraza lake la mawaziri, wa hivi punde akiwa mgombea urais wa zamani aliyemtaka aitaje baraza lake haraka iwezekanavyo.
Habari Nyingine: 'Maceleb' 17 ambao wanafanana kwa sura ila hawana uhusiano wowote
Ekuru Aukot alimtaka Uhuru kumuiga mwenzake George Opong Weah, wa Liberia aliyelitaja baraza lake siku chache tu baada ya kuapishwa.

Habari Nyingine: Sosholaiti Vera Sidika amtambulisha mpenziwe mpya kwa umma, pata kumfahamu
"Tunashangaa ni kwa nini Uhuru Kenyatta amechukua miezi mitano tangu Agosti kutambua watu wa kujumuishwa katika baraza la mawaziri," Aukot.
Wengi wamekuwa wakilalama kuwa Uhuru amekaa sana kabla ya kulitaja baraza lake la mawaziri ikizingatiwa aliapishwa siku kadha zilizopita.
Hata kabla Aukot amalize kusema hayo, Rais Uhuru amelitaja baraza hilo.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Wafuasi wa NASA wahimizwa kususia bidhaa za kampuni ya Haco Tiger – Kwenye TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4Fzg5dmq66mkai1orrGmphmppliuLitjKegp6FdqrW2vtRmmKadk53CrMHAZqSimZuWeq%2BtjKagpJmblnqswcuiq5qikWKvor7As5hmpJGgsm64wGakmq%2BRr7aztYyeoq6qpWKutrfOrWWhrJ2h